Burudani

Rihanna asaini dili nono la shilingi bilioni 54 na Samsung kudhamini album yake mpya

Rihanna akiwa anajiandaa kutoa album yake mpya, amesaini dili nono la dola milioni 25 (sawa na shilingi bilioni 54) na kampuni ya Samsung kwaajili ya kudhamini album hiyo pamoja na ziara.

rihanna-shades

Jay Z pamoja na meneja wa Rihanna, Jay Brown walisaidia katika kufunga dili hiyo.

Mapema mwezi huu Jay Z alionekana akitoka kwenye ofisi za Samsung na kudhaniwa alienda kwaajili ya TIDAL, lakini inasemekana alienda kujadiliana kuhusu dili ya Rihanna ambaye yuko chini ya Roc Nation.

Kupitia udhamini huo, Samsung wamepanga kumtumia Riri kupromote bidhaa zao za Galaxy na watahitaji watumie video zote zinazomuhusu Rihana exclusive kwenye app yao ya Milk Music App.

Roc Nation imejenga uhusiano mzuri na kampuni hiyo kwa muda sasa, mwaka 2013 kampuni hiyo ya Korea ilinunua nakala milioni moja za album ya Jay Z, ‘Magna Carta… Holy Grail’ na kuisambaza bure kupitia simu zake za Galaxy.

Rihanna bado hajatangaza tarehe rasmi ya kuachia album yake ya nane, ‘Anti’ lakini inatarajiwa kutoka kabla mwaka huu haujaisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents