HabariMichezo

Ronaldo asujudu uwanjani baada ya kufunga goli la ushindi

Mshambuliaji wa klabu ya Al Nassr kutoka nchi Saudi Arabia na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amesujudi uwanjani baada ya kufunga goli la 3 na la ushindi dhidi ya klabu ya Al Shabaab katika ligi kuu nchini Saudi Arabia.

Kitendo hicho cha kusujudu kimetafsiriwa na wengi huenda Ronaldo amesilimu (Amekuwa Muislamu) kwani kitendo hicho hufanywa na Waislamu kama ishara ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kile alichokupatia au kumuomba akupatie kitu fulani.

Cristiano Ronaldo amefunga goli la 3 na kuifanya klabu yake kushinda kwa jumla ya goli 3-2 baada ya kuwa nyuma kwa goli 2-0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents