Habari

RPC asimulia tukio la mwizi aliyeganda na mzigo ‘tulijaribu kuutoa mzigo tukashindwa’

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shanna ameelezea jinsi walivyomtua mzigo mwizi aliyeganda na kiroba cha mahindi alichoiba huko Mlandizi Kibaha.

Mapema leo kijana huyo aitwae, Frank Joseph mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Mbezi alijisalimisha polisi baada ya kuiba mzigo wa mahindi na kushindwa kuutua.

Kamanda Polisi amesema baada ya kijana huyo kumuona walifanya naye mahojiano na kukiri kuiba mzigo huo na kila walivyojaribu kuuondoa mzigo huo kijana huyo alipiga kelele za maumivu hali ambayo iliwafanya wamuache na kumtafuta mtu aliyeibiwa.

“Mnamo tarehe 3 mwezi wa tano mwaka 2018 majira ya saa 12 na dakika 45, huko katika kata ya Mlandizi Wilaya ya Kibaha na mkoa wa Pwani tulipata taarifa toka kwa mwenyekiti wa Mlandizi ndugu Ally kwamba kuna mtu asiyefahamika amekutwa amebeba mahindi yanayokadiriwa kuwa na uzito wa kilo 20 na ameshindwa kuyatua toka kichwani na wakati huo huo akaendelea kutueleza kwamba amezungukwa na watu wenye hasira wanataka kumuadhibu. Baada ya kupata taarifa hiyo tulifika eneo la tukio na kukuta kweli mtu huyo yupo na amebeba mahindi, tulimuamuru azitue chini lakini akashindwa na pia tukajaribu kumtua lakini tukashindwa kutokana na kelele za maumivu alizokuwa akizitoa,” alisema Kamanda.

Baada ya zoezi hilo kushindikana jeshi la polisi lilimwita mtua ambaye anadaiwa kuibiwa na kufanya manjonjo yake na muda mchache akamtua kijana huyo zigo la mahindi.

Polisi wamesema kwa sasa wapo kwenye jitihada za kumpandisha kizimbani kijana ambapo pia wamewataka wananchi kuepuka matukio ya kihalifu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents