Burudani

Bill Nass ‘akata mzizi wa fitina’ kuhusu Alikiba

Bill Nass anarudi kwenye headlines za kiburudani kwa mara nyingine tena, sasa hivi ni kuhusu yeye na Alikiba.

Rapper huyo ambaye anatamba na ngoma ‘Tagi Ubavu’ amefunguka kuhusu tetesi zilizodai kuna ngoma kati yake na Alikiba inakuja.

“Sitaki kuliweka sana hilo mbele ila watu wajue tunayo mahusiano mazuri kama nilivyo na mahusiano mazuri na wasanii wengine,” Bill Nass ameiambia Kikaangoni, EATV.

Utakumbuka Mr. Blue, Mwana FA na Godzilla ni miongoni mwa wasanii wanaofanya muziki wa rap ambao waliweza kumshirikisha Alikiba katika ngoma zao na aliweza kuzitendea haki kwa upande wa chorus.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents