Burudani

Sababu ya Amber Lulu kujiachia, ‘familia yangu haifuatilii mitandao’

Msanii wa muziki na video vixen Bongo, Amber Lulu amedai kuwa familia yake haifuatilii mitandao hivyo yupo free kujiachia kwa kuweka picha anazotaka.

Video Vixen huyo ambaye ameingia kwenye muziki wa Bongo Flava na kutoa ngoma ‘Watokoma’ ambayo alimshirikisha Country Boy, ameiambia Leo Tena ya Clouds Fm kuwa hata familia ikiona picha zake hamna tatizo.

“Familia yangu hawafatilii mitandao ya kijamii na hata wakiona picha zangu kwa sasa wanaelewa nini nafanya. Siyo kila kitu tunachoposti kwenye mitandao ya kijamii ndivyo maisha yetu tunayoishi” amesema Amber Lulu.

Kabla ya kuingia katika muziki na kutangaza kuachana na u-video vixen, Amber Lulu alishatokea kwenye video kama Inde ya Harmonize na Dully Sykes, Usimsahau Mchizi ya Roma na Moni n.k.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents