Burudani

Sababu ya Diddy kumpiga Drake yafahamika, ni ugomvi juu ya wimbo

Siku mbili zilizopita kulikuwa na ripoti kuwa Diddy alimpiga Drake kwenye club ya Miami Jumatatu wiki hii, lakini sababu ilikuwa haijawa wazi licha ya baadhi ya ripoti kuwa chanzo ni mpenzi wa Diddy aitwaye Cassie.

drake n Diddy

Kwa mujibu wa TMZ, inasemekana kuwa sababu halisi ya ugomvi huo ni wimbo wa Drake “0 to 100/ The Catch Up”.

Vyanzo vimesema kuwa producer Boi-1da aliugawa wimbo huo kwa wote wawili Diddy na Drake miezi nane iliyopita na Diddy alikuwa tayari ameurekodi, kitendo ambacho kilimkera Drake kwasababu naye alikuwa anataka kuurekodi.

Drake naye aliamua kwenda kurekodi wimbo huo sehemu nyingine na kuutoa July 15,2014 na kufanikiwa kufanya vizuri hadi umepata nomination mbili kwenye tuzo za Grammy 2015 kitendo ambacho kilimuudhi Diddy.

“0 to 100/ The Catch Up” imeingia kwenye kipengele cha Best Rap Performance na Best Rap Song.

Inadaiwa kuwa baada ya Diddy kumuona Drake Jumatatu walipokutana kwenye birthday ya DJ Khalid ilikuwa ni mara ya kwanza kuonana toka Drake auachie wimbo huo. Vyanzo vya karibu na Diddy vimesema kuwa Diddy alimfuata Drake ambaye alimjibu kijeuri na ndio chanzo cha Diddy kusema “You’ll never disrespect me again,” na kilichofuatia ni kumpiga konde moja.

Inasemekana baada ya kushushiwa kichapo Drake aliishia hospitali kwasababu katika purukushani hizo alitoneshwa kidonda chake begani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents