Burudani
Saraha kuingia kwenye mashindano makubwa ya Sweden kutangaza muziki wa Kiswahili
Muimbaji wa nchini Sweden, Saraha aliyewahi kuishi Tanzania kwa miaka kadhaa anatarajia kushiriki kwenye mashindano makubwa nchini kwao.
Amesema kupitia mashindano hayo, atautangaza muziki wa Kiswahili.
Kupitia Facebook, Saraha ameandika, “Tarehe 20 natoa wimbo wangu mpya – Kizunguzungu! Nitaingia mashindano maarufu na makubwa ya muziki nchini Sweden! Nimepata nafasi kubwa ya kutangaza mziki wangu na mziki ya Kiswahili.”
Saraha alirudi Sweden baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, Fundi Samweli.