Burudani

Scandal ya passport ya Jose Chameleone yampandisha chart nchini Tanzania


Umaarufu wa Jose Chameleone nchini umeongezeka maradufukutokana na scandal ya kushikiliwa passport yake na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Global Publishers, Erick Shigongo.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Bongo5 kwenye radio za hapa nchini, wimbo wake mpya wa Valu Valu, umekuwa ukiombwa zaidi na wasikilizaji kuliko kawaida.
Wale waliokuwa hawaujui wimbo huo pia, sakata hilo limewafanya waufahamu wimbo huo ambao kwa sasa umekuwa club banger kila kona.
Kufuatia kushikiliwa kwa passport yake kwa wiki kadhaa na Shigongo aliyedai kutapeliwa na meneja wa msanii huyo, wiki iliyopita Chameleone aliandamana kwenye ubalozi wa Tanzania mjini Kampala Uganda kudai arejeshewe.
Tukio hilo liliripotiwa na vyombo vingi vya habari vikiwemo vya kimataifa na hivyo kusaidia kurudishiwa passport yake.
Weekend hii kupitia Facebook, msanii huyo aliandika:
“Back to business. 3rd August Dr Chameleone live in South Africa.27th August Wembley arena London, Africa Unplugged.First September Miss East Africa Brussels am here.Norway,Sweden,Switzerland,France,Denmark, DR Congo and Malawi! i c u thru.i got my rights back i will be there!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents