Habari

Sean Paul alichagua kwenda Uganda badala ya Kenya sababu wakenya waliiba simu yake

Inaonekana kama vile mwanamuziki wa dancehall wa Jamaica, Sean Paul hajasahau jinsi wajanja wa Kenya walimvyomliza simu yake alipokwenda kupiga show jijini Nairobi.

Hiyo ndio sababu ya mshindi huyo wa tuzo za grammy Sean Paul Ryan Francis Henriques kuamua kwenda kupiga show November 9 jijini Kampala, Uganda badala ya Kenya kwa hofu kuwa anaweza kuibiwa tena.

Staa huyo anadai kuwa aliingia hasara kubwa kupoteza simu yake sababu ilikuwa na contacts za maceleb kibao kama Beyonce na wakenya wangeweza kuitumia simu hiyo vibaya.Hatujui kama namba ya simu ya Beyonce aliipata tena!

Kwa mujibu wa vyanzo, ni ngumu sana kwa mapromota kumshawishi msanii huyo kufanya tena show nchini Kenya.

Hivi karibuni msanii mwingine wa Jamaica, Tarrus Riley aliibiwa simu yake pia jijini Nairobi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents