Habari

Serikali haifanyi kazi kwa miujiza -Muhagama

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema serikali ya awamu ya tano haifanyi kazi kwa miujiza bali huafanya kazi kwa mpangilio wa bajeti iliyojiwekea.

imgs0705

Ametoa kauli hiyo Jumannne hii kwa niaba ya Waziri Mkuu wakati akijibu swali la mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, lililoihoji serikali kuhusu kutekeleza ahadi milioni 50 kwa kila kijiji kama serikali ya awamu ya tano ilivyoahidi.

Swali la Mbowe lilikuwa: Je, ni muujiza gani itakayotumiwa na serikali hii ambayo leo imefilisika,ambayo leo imeshindwa kutoa mikopo ya wanafunzi wa chuo kikuu kwa maelfu, kwahiyo nauliza ni miujiza gani serikali ambayo imefilisika itakayotumia kutafuta fedha hizi bilioni 960 baada ya kuwadanganya wananchi?

Katika jibu lake, Mhagahama alisema: Naomba kuwahakikishia waheshimiwa wabunge kwanza serikali hii haifanyi kazi kwa miujiza. Serikali hii inafanya kazi kwa mpangilio wa bajeti iliyojiwekea. Nina uthibitisho wa kwamba jambo hili linatekelezeka ni kama tulivyoweza kuwashangaza watanzania kwa kutoa elimu bure kwa mabilioni ya fedha.”

Aliongeza, “Tulivyoweza kuwashangaza Watanzania kwa kutekeleza miradi mingine mikubwa hata ununuaji wa ndege,tulivyoweza kuwashangaza Watanzania kwa utekelezaji wa ilani yetu kwa mambo mengine mbalimbali, ninaomba niwathibitishie watanzania fedha hizi zitatolewa na watanzania watazipata. Na serikali hii haitafanya kazi kwa miujiza, itafanya kazi kwa mpango wa utekelezaji wa bajeti za wananchi tuliyojiwekea na fedha hizo zitafika hata kwa majimbo pinzani katika nchi ya Tanzania.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents