Habari

Serikali yaendelea kupigilia misumari suala la wanafunzi waliopata ujauzito kurudi shule

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha imesema kuwa haitarajii kuwarudisha wanafunzi waliopata ujauzito shuleni kwa njia yoyote ile.

Akizungumza leo, Bungeni mjini Dodoma, Nasha amesema kuwa ukiruhusu hilo ni mwanzo kuhamasisha ngono mashuleni wakati mila na sheria zetu haziruhusu ngono katika shule.

“Hata sisi serikali kwa kweli hatupendi kusikia vitendo vya uonevu dhidi ya watoto wa kike kwasasa mfumo wetu wa elimu umepangwa katika namna ya kuhakikisha wanafunzi wanafunzi wanaopata ujauzito wanapata fursa ya kuoa lakini nje ya mfumo rasmi kwahiyo kuna fursa nyingine nyingi za kusoma kama nilivyosema katika swali langu la msingi kupitia elimu ya watu wazima lakini vilevile vyuo vya ufundi,“ amesema Nasha.

“Serikali haitarajii na naomba niweke wazi wanafunzi ambao wamepata ujauzito kwa njia yoyote ile na kwasababu ukifanya hivyo ndio maana yake una halalisha na kuhamasisha ngono mashuleni wakati mila zetu na sheria zetu haziruhusu ngono katika shule maana yake katika shule za msingi na sekondari.“

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents