Habari

Serikali yatoa kauli juu ya ulipaji wa madeni ya walimu

Serikali imesema kuwa suala la uhakiki wa madeni kwa walimu limekwisha ambalo lilikuwa changamoto sasa walimu hao wataanza kulipwa muda si mrefu.

Hayo yamesema Ijumaa hii mjini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo, kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI, alipokuwa akijibu swali la mbunge Benadeta Mshashu lililohoji, Je, serikali italipa lini madeni ya walimu? sambamba na mbunge huyo akitaka kutajiwa tarehe.

“Kama nilivyosema awali kwanza tuweke reference vizuri hapa na kumbukumbu vizuri katika kada ambayo serikali katika njia moja au nyingine imekuwa ikishiriki vizuri katika ulipaji wa madeni ni kada ya walimu. Ukiangalia miaka mitatu mfululizo trend ya madeni ya walimu tumekuwa tukizungumza hapa katika Bunge kila wakati, kwa kweli serikali inafanya kazi sana na ndio maana hata kwa kipindi cha sasa ukiangalia mwezi wa 11 huu uliopita kuna baadhi ya madeni ya walimu katika baadhi ya wilaya kwa mfano kuna halmashauri ya Temeke na halmashauri zingine kulikuwa na deni kama la bilioni 1 nalo lililipwa vilevile,” amesema waziri Jafo.

Ameongeza “Maana katika ulipaji wa madeni haya, haya madeni mapya mengine na ndio maana serikali ilikuwa inafanya zoezi hili zima la uhakika vizuri, ofisi ya TAMISEMI pamoja na HAZINA jambo hili limekamilika siwezi sema deadline lini hilo deni litalipwa, lakini kwasababu mchakato wa uhakiki umekamilika hili deni la shilingi bilioni 26 naamini muda si mrefu Hazina mchakato wa malipo utaanza kuanza. Naomba nikwambie mheshimiwa mbunge najua uko makini katika hili lakini amini serikali yako kwamba kwa vile zoezi la uhakiki lililokuwa changamoto limekamilika basi walimu hao wataanza kulipwa muda si mrefu.”

Na Emmy Maipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents