Burudani

Shaa azungumzia kula Christmas bila mama yake, ‘alipendelea kufurahisha wengine na yeye kujinyima’

Hii ni mara ya kwanza kwa Sarah Kaisi aka Shaa kusherehekea sikukuu ya Christmas bila kuwepo mama yake aliyefariki August mwaka huu.

shaa sugua gaga

“Christmas ya kwanza bila msosi wa mama…company yake…kwake yeye sikukuu ni muda wa kushare baraka za Mola..alipendelea kufurahisha wengine na yeye kujinyima…kwangu mimi, hii ndiyo maana haswa ya Christmas…Nitakukumbuka milele Mama…Christabella Octavia Kaisi,” ameandika Shaa kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mwishoni mwa mwezi August mwaka huu, Shaa aliiambia Bongo5 kuwa kumpoteza mama yake mzazi kumemwacha katika wakati mgumu kwakuwa alikuwa akimchukulia mama yake kama role model na ndiye aliyemjenga kuwa Shaa mwanamuziki.

“Kutokana na kumuuguza muda mrefu, kidogo imenifariji kwamba amepumzika lakini bado inauma kwamba natamani bado angekuwepo na mimi lakini inshallah ni mipango ya Mungu, amenitangulia tu wote tunaenda huko huko,” alisema Shaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents