Picha
Elizabeth Gupta na mumewe Pam (mshindi BBA4) wafungua mgahawa Nigeria ‘Gupsy’s Delight’
Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa msimu wa 4 (Revolution) Elizabeth Gupta na mumewe Kevin Chuwang Pam (mshindi wa BBA4) wamefungua mgahawa wao nchini Nigeria.
Mgahawa huo uitwao ‘Gupsy’s Delight’ upo jijini Lagos, Nigeria ambako Liz na Pam wanaishi. Kupitia Instagram, Gupta ameonesha picha za mgahawa huo.
Kwa sasa mastaa hao wana familia ya watoto wawili.