Promotion

Instagram Party kufanyika Ambassadors Lounge kwenye Boxing Day, Hisia (TPF6) kutumbuiza

Instagram Party ni tukio la kiburudani linaloandaliwa na kampuni ya Freconic Ideaz Entertainment. Ni tukio mashuhuri linalokusudia kuwakutanisha,kuwaunganisha na kuwaburudisha watumiaji wa mitandao ya kijamii hususani Instagram.

IMG_21786833530542

Ni tukio la aina yake kuwahi kutokea hapa Tanzania kwa maana Instagram imekua ni kivutio kikubwa kwa
vijana wa karne hii ya sayansi na teknolojia ambao wengi wamekua wakiambatana na fursa zitokanazo na mabadiliko ya Teknohama. Instagram ni ‘habari ya mjini’ kama vijana wasemavyo ikimaanisha kwamba ni swala linalotupiwa jicho na watu wengi sana hivi sasa.

Kwa kuliona hitaji kubwa la aina hii ya burudani kampuni kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa burudani imeoekana ifanyike party hii ya aina yake katika usiku wa tar 26 ‘boxing day’ ambapo watumiaji wengi na wadau mbalimbali wa burudani wataweza kukaribia Ambassadors Lounge Benjamin Mkapa tower posta mpya kukutana,kufahamiana zaidi,kubadilishana mawazo na kufurahi kwa pamoja kupitia burudani mbalimbali zitakazo kuwa zikiendelea.

HISIA ambaye ni mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Tusker Project Fame 6 lililokwisha hivi karibuni anapewa nafasi ya kuwaburudisha watanzania kwa mara ya kwanza akidhihirisha kipaji chake,kutakuwa na suprise za nyota wanaokubalika katika tasnia ya sanaa nchini Tanzania. Huku kukiwa na Red carpet watu mbalimbali ikiwemo watu mashuhuri watapata fursa ya kupita hapo na kumbukumbu za picha pamoja na ‘interviews’ vitachukua nafasi.

Utofauti wa tukio hili na matukio mengine yaliyotangulia ni kwamba maandalizi yanayokidhi haja yamefanyika,wakati muafaka umezingatiwa na timu ya maandalizi ni ya watu wenye uzoefu mkubwa katika maswala ya burudani hivyo basi yale matarajio ya wahudhuriaji yatatendewa haki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents