Shahidi kesi ya Sabaya athibitisha kutoa millioni 90 kwenye boksi

Kesi ya Uhujumu uchumi Na.27/2021 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, imeendelea leo ambapo Meneja wa Benki ya CRDBA ameweka wazi kuwa aliidhinisha kiasi cha milioni 90 kutolewa kwenye Akaunti ya mteja wao, Francis Mroso.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dk. Patricia Kisinda, Shahidi ambaye ni Meneja wa benki tawi la kwa Mromboo Jijini Arusha, amesema akiwa kama mwangalizi alihakikisha milioni 90 zimewekwa ndani ya boksi na kukabidhiwa kwa Mteja.

Shahidi huyo amesema alishtushwa na kitendo cha mteja wao kutoa kiasi kingi cha fedha kwa kuwa hakuwa na utaratibu wa kutoa pesa mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kutoa kingi cha fedha.

Shahidi ameilezea mahakama kuwa hata alipotaka kujua sababu ya mteja huyo kutoa pesa nyingi kwa mara moja alimjibu kuwa anataka kumlipa mtu na hata alipomshauri mteja wake (Mrosso) asitoe ‘Cash’ na badala yake alipe kwa kuhamisha kwenye akaunti ya mdeni wake, alimuomba yeye (meneja ) azungumze nae ingawa juhudi zake za kumshawishi (mdeni) kufungua akaunti ziligonga mwamba baada ya kujibiwa kwamba akaunti atafungu siku nyingine na siku hiyo alihitaji alipwe kwa ‘Cash’.

Shahidi ameeleza mahakama kwamba baada ya kushindwa kumshawishi mteja huyo yeye kama msimamizi wa bank aliidhinisha pesa hiyo kutoka kwa Akaunti ya Mrosso kutolewa na kukabidhiwa kiasi cha milioni 90/kwenye boksi.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka kesho Novemba 17, ambapo Hakimu Kisinda anatarajiwa kutoa maamuzi madogo ya pingamizi yaliyotolea na upande wa utetezi.

BY: Fatuma Muna

 

Related Articles

Back to top button