Habari

Shosteez kuachia wimbo mpya ‘Nifikirie’ wiki ijayo, umeandikwa na Q-Chief na Cassim

Kundi la wasichana watatu la Shosteez lililochini ya uongozi wa producer Lamar linatarajia kuachia single mpya na ya pili wiki ijayo. Kundi hilo linaundwa na Menina, Salma na Nuru.

29
Nuru

Akiongea na Bongo5, Lamar amesema wimbo huo wa Kiswahili na ulioandikwa na Q-Chief pamoja na Cassim Mganga unaitwa Nifikirie.

26
Salma
Lamar ambaye ameutengeneza wimbo huo amesema Nifikirie ipo katika mahadhi ya Afro-Pop na Zouk ana amedai kuwa video ya wimbo huo anaifanya mwenyewe.

13
Menina

Wakati huo huo, Lamar amesema ameongeza producer mwingine aitwaye Rodgers ambaye mpaka sasa ameshatengeneza nyimbo nne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents