Michezo

Sir Bobby Charlton amkabidhi Wayne Rooney tuzo ya heshima Man United

Sir Bobby Charlton jana Januari 29 wakati wa mchezo wa FA Cup dhidi ya Wigan katika uwanja wa Old Trafford amemkabidhi Wayne Rooney tuzo ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Man United.

Januari 21, 2017, mshambuliaji wa kimataifa wa England Wayne Rooney alifunga bao ambalo lilikuwa la kusawazisha na kuipa timu yake ya Manchester United pointi moja katika mchezo dhidi ya Stoke City baada ya kufungana bao 1-1. bao hilo lilimfanya mchezaji huyo afikishe mabao 250 na kuwa mfungaji kinara wa muda wote katika klabu ya Manchester United.

Rooney alifunga bao kwa mpira wa adhabu (free-kick) akimtungua mlinda mlango wa Potters Lee Grant kwa bao lake la 250 akiwa na United, bao moja zaidi ya mkongwe wa klabu hiyo aliyeshikiria rekodi hiyo kwa muda mrefu Sir Robert ‘Bobby’ Charlton CBE.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents