Habari

Sitofanya Uasi baada ya mke wangu kufariki – Mrema

Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema, amesema hatafanya uasi wa aina yoyote baada ya mkewe Rose Mrema kuaga dunia.

Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema, akiwa na mke wake Rose Mrema, enzi za uhai wake

Mrema ameeleza hayo leo Oktoba 04, akiwa nyumbani kwake Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni siku chache kupita tangu kufariki kwa mke wake.

Nikisema ‘na-mmiss na-mmiss’ kweli, nimekubaliana na mke wangu sitafanya uasi wowote baada ya yeye kufariki. Nitafata nyayo zake. Kabla ya kufariki alituita kwa pamoja na watoto na wajukuu na kutuweka sawa. Watoto walikuwa wanakwaruzana lakini tumesikia na tutayaenzi yote ya mama,” Mrema.

Aidha Mrema amesema kabla ya Mkewe kufariki amemfanyia mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kumuunganisha na Serikali na ndio sababu hata alipofariki aliweza kupokea salamu za rambi rambi kutoka kwa Rais na Waziri Mkuu

Bi. Rose Mrema, alifariki dunia Septemba 16, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia kupatwa na tatizo la shinikizo la damu, ambapo taarifa ya madaktari ilisema mishipa mitatu ilikuwa imeziba kwa muda mrefu.

BY : Fatuma Muna

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents