Burudani

Staa huyu mkubwa wa muziki duniani alikuwa hajui tango lilivyo tangu azaliwe

Staa wa pop wa nchini Uingereza, Robbie Williams hakuweza kulitambua tango kwasababu tangu azaliwe amekuwa akilila likiwa limemenywa tu.

Williams

Mke wa staa huyo aliyepata umaarufu akiwa na miaka 16 tu kupitia kundi lake la Take That aliishi maisha ya ustaa kiasi ambacho alishindwa kutambua zao hilo alipolikuta likiwa zima kwenye friji.

“Siku moja nilitoa tango kutoka kwenye friji na aliniuliza nini hicho. Alisema alikuwa halijui sababu amekuwa akiliona likiwa limemenywa tu,” alisema mke wake.

“He’s only had them in salads when they’ve been sliced for him. He’s not used to see them in full form,” aliongeza.

Mke wake Ayda Field ambaye ni muigizaji, alisema maisha ya kitajiri na umaarufu kwa mumewe yamekuwa na madhara katika masuala ya kawaida ya nyumbani. Alikuwa akizungumza kwenye kipindi cha runinga cha ‘Loose Women’ na kudai kuwa mumewe hajui hata kubadilisha bulb nyumbani. “God no! He doesn’t know how to change a lightbulb,” alisema.

Hivi karibuni Ayda alidai pia kuwa muimbaji huyo wa ‘Let Me Entertain You’ alienda supermarket kwa mara ya kwanza katika maisha yake mwaka huu na alishangaa alichoona.

“He is 42 and for the first time he went to the supermarket the other day. He’s like a 15-year-old boy, he’s frozen in Take That time. He was like, ‘this is amazing, they’ve got everything. I was like, ‘that’s what you do at the supermarket!’ It was a revelation.”

Wawili hao wana watoto wawili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents