Habari

Super Sports kurusha live mechi za ligi kuu Tanzania bara

Kituo maarufu cha runinga cha Supersports (DSTV) kinachosifika kwa michezo barani Afrika, kinatarajia kurusha live mechi za ligi kuu soka Tanzania bara kwa mara ya kwanza.

Tayari crew nzima ya Super Sports imekwisha wasili nchini huku ikiwa na watangazaji na wachambuzi wake maarufu wa mechi mbalimbali za kimataifa.

Super Sports itaonesha jumla ya mechi tano live za ligi kuu soka ya Tanzania bara.

Akiongea na Clouds FM leo kwenye kipindi cha Power Breakfast mmoja watangazaji wa kituo hicho Thomas Mlambo amesema lengo la Super Sports kuonesha ligi kuu ya Tanzania bara ni kutokana na kiwango cha uchezaji katika ligi hiyo kuongezeka na wengependa kukionesha kwa mataifa mengine duniani.

Miongoni mwa mechi zitakazooneshwa ni pamoja na ile kesho Ijumaa kati ya Azam FC na JKT Ruvu itakayochezwa saa moja jioni, Simba na Tanzania Prisons siku ya Jumamosi na ile ya Yanga na African Lyon itakayochezwa Jumapili hii zote kwenye uwanja wa taifa.

Pia wiki ijayo kituo hicho kitarusha live pambano la watani wa jaji Simba na Yanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents