Burudani

Taarifa: Kwanini Bongo5.com haishiriki kwenye Tuzo za watu 2015

Tungependa kutoa taarifa kwa wapendwa wasomaji wetu ambao wamekuwa wakituuliza maswali ya kwanini bongo5.com haijaingia kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za Watu 2015 licha ya kuipendekeza kwa wingi.

11192681_961039440597522_1774392183_n

Ni kweli bongo5.com ina wasomaji wengi na wasomaji wetu waliipendekeza kwa wingi ili iingie kuwania kipengele cha Blog/Website inayopendwa. Kutokana na mapendekezo mengi, bongo5.com ilifuzu kuingia kwenye top 5. Tunashukuru kwa hilo.

Hata hivyo kwakuwa kwa mwaka huu Bongo5 Media Group ambao ni wamiliki wa bongo5.com ni mmoja kati ya waandaji wa tuzo hizo, imelazimika kuitoa bongo5.com kuwania kipengele hicho na kuipa nafasi blog nyingine iliyopendekezwa nyuma ya tano za mwanzo.

Tunafahamu kuwa wapo baadhi ya wasomaji wetu waliotamani kutuona pia tukiwania tuzo, hivyo tunawaomba radhi kwa kutoweza kushiriki kutokana na sababu hizo. Tumefanya hivyo ili kuonesha ni kwa kiasi gani Tuzo za Watu ni tuzo makini na zenye uwazi mkubwa.

Asante kwa kuendelea kuwa msomaji wetu mzuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents