Burudani

Taarifa: Uhalali na uwazi wa kura za Tuzo za Watu

Tungependa kutoa taarifa kuelezea baadhi ya duku duku zilizojitokeza miongoni mwa wananchi kuhusiana na uhalali wa majina yaliyoingia kwenye tano bora ya tuzo za watu kutokana na mapendekezo ya wananchi.

TUZO

Baadhi ya wananchi wamekuwa wakionesha wasiwasi kuhusiana na majina yaliyoingia kwenye tano bora kwa kuona kuwa baadhi ya majina waliyoamini yalitakiwa kuingia hayamo.

Tunapenda kuwahakikishia kuwa zoezi la kukusanya mapendekezo hayo lilikuwa wazi na limefanywa kwa usimamizi kutoka mwakilishi waa Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA aliyeshuhudia idadi ya kura zilizopigwa na kushuhudia zikihesabiwa. BASATA ndio chombo kilichotoa kibali cha kufanyika kwa tuzo hizi.

Baada ya hatua hiyo ya kwanza ya kukusanya mapendekezo hayo, kampuni tuliyoipa dhamana ya kukagua kura hizo ya Deloitte ilipitia mapendekezo kwa mara nyingine na kujiridhisha kuwa majina yaliyopata kura nyingi ndio yaliyoingia kwenye tano bora.

Hakuna jina lililoingizwa kwa kuchaguliwa na mtu mwingine zaidi ya nguvu ya mapendekezo ya wananchi.

Kama tulivyowahi kueleza awali wakati tunaanzisha tuzo hizi, washindi wa Tuzo za Watu wanapatikana kwa asilimia 100 ya kura za wapiga kura. Mwenye nguvu ya kupata kura nyingi zaidi ya wengine ndiye atakayekuwa mshindi, hakuna njia nyingine!

Sisi kama moja ya waandaji, tunachokifanya ni kusimamia tu vigezo vilivyowekwa katika kila kipengele na kuhakikisha kuwa majina yaliyoingia kwenye tano bora yamekidhi vigezo hivyo.

Tunawaomba wananchi kuwa na imani na sisi. Tunawaomba wananchi kuwa na imani na tuzo hizo kwakuwa ni kweli hizi ni tuzo za watu.

Tupo tayari kuonesha matokeo ya kila hatua inayofuata ili kuonesha uwazi wa tuzo hizi na kwamba kila atakayesonga mbele kwenye hatua nyingine amefanikiwa kutokana na wingi wa kura alizozipata.

Tunawahakikishia pia kuwa washindi watakaopatikana watatokana na asilimia 100 ya kura zilizopigwa na mashabiki wao. Hakuna mshindi atakayepatikana kwa njia nyingine zaidi ya kura yako.

Hivyo tunaomba muendelee kuyapigia kura majina mnayopenda yashinde.

Tunashukuru kwa ushiriakiano mnaotupa hadi sasa. Asanteni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents