Michezo

Taasisi ya Didier Drogba kikaangoni kwa kula fedha za wahisani!

Ni asilimia 1 katika paundi milioni 1.7 zilizochangwa na mastaa na wafanyabiashara wa Uingereza kwaajili ya kuisaidia taasisi iliyoanzishwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, zimewafikia walengwwa, imebainika.

Drogba

Taasisi hiyo inayosaidiwa pia na Princess Beatrice na David Beckham inachunguzwa. Wachangiaji wakiwemo Bono, Frank Lampard na Christine Bleakley, waliambiwa kuwa fedha hizo zingetumika kujenga hospitali na kuwapa elimu watoto maskini nchini Ivory Coast.

Lakini Mail Online imeripoti kuwa ni £14,115 tu ndizo zilizowafikia walengwa. £439,321 zilitumika kuandaa hafla ya kifahari ya uchangiaji iliyopambwa na burudani za muziki kutoka kwa wasanii wakubwa.

Mastaa wengine wanaoisaidia taasisi hiyo ni pamoja na Pele, John Terry, Roger Federer na Donna Air, girlfriend wa kaka yake na Duchess of Cambridge, James. Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich naye alidaiwa kuchangia kiasi kikubwa cha fedha.

Pia kuna maswali kuhusu fedha za udhamini kutoka kwa makampuni kama Pepsi, Nike ma Samsung, ambazo Drogba alidai zimeenda kwenye charity.
SOMA ZAIDI HAPA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents