HabariSiasa

Taifa la Oman lasherehekea miaka 52 tangu kuasisiwa kwake

TAIFA la Oman leo Ijumaa ya Novemba 18 Novemba, 2022 linasherehekea miaka 52 ya kuasisiwa kwake pamoja na mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa katika muamko wake Mpya, na kipindi chake kitukufu, chini ya uongozi wa Mtukufu Sultani Haitham bin Tariq.

Kiongozi ambaye amekuwa akifanya juhudi kubwa bila kuchoka katika kuimarisha nafasi na hadhi ya Dola ya kisasa, kimaendeleo na kiuchumi, na ili kila Mwananchii wa Oman awe
mshiriki wa kweli wa maendeleo jumuishi.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo imefafanua kwa kina mafanikio ya Taifa hilo ambalo linasheherekea miaka 52 ya kuasisiwa kwake huku ikielezwa hatua kwa hatua mageuzi yanayoendelea sasa hivi Oman, kuelekea kwenye mfumo wa kidijatali wa Serekali, ni moja ya programu za utekelezaji wa uchumi wa kidijiti, na moja ya nyenzo kuu za kusaidia kufikia vipaumbele vya Dira ya “Oman 2040 “.

Kwa mujibu wa taarifa kwamba Mtazamo wa Mtukufu Sultani unajipambanua kama maono ya busara na yanayoangalia mbali kwani umejikita katika kuendeleza azma ya Oman ya kuwa na ushirikiano chanya na wote na katika nyanja anuwai zenye manufaa, na kwa namna ambayo itakuza masilahi ya pande zote, na matokeo ya mtazamo huo yamejitokeza katika ziara za viongozi mbalimbali duniani akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibari Dkt. Hussein Ali Mwinyi Raisi wa Zanzibar, ziara ambazo zimefikia kilele chake kwa kuanzishwa ubia wa aina mbalimbali na kusiniwa hati za maelewano na mipango ya utekelezaji katika nyanja kadhaa zikiwemo za uwekezaji na biashara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents