Habari

Tanzania yaendelea kung’ara Urusi, yatinga kibabe nusu fainali ya kombe la Dunia

Timu ya Wasichana ya Tanzania inayoundwa na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kutoka kituo cha TSC cha jijini Mwanza leo alfajiri wameibuka na ushindi wa goli 5–0 dhidi ya Marekani kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia la Watoto wanaoishi mazingira magumu na kufanikiwa kutinga nusu fainali.

Timu hiyo pekee kutoka Tanzania mpaka sasa haijapoteza wala kuruhusu goli katika katika michezo mitatu iliyocheza kwenye michuano hiyo ya kombe la dunia.

SOMA ZAIDI – Timu ya wasichana ya Tanzania yang’ara kombe la Dunia Urusi

Timu hiyo ya Wasichana kutoka Tanzania ambao ndiyo mabingwa watetezi wa kombe la dunia, sasa watavaana na timu ya wasichana ya Uingereza kwenye mchezo wa nusu fainali baada ya Uingereza kuifunga Bolivia mabao 2-0.
Mchezo huo utapigwa kesho Mei 13, 2018 saa 3:30 asubuhi kwa saa za Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents