Habari

Tanzia: Brigedia Jenerali (mstaafu) Albert Costantino Frisch afariki dunia

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu) kilichotokea tarehe 13 Aprili 2017.

Marehemu Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu) alizaliwa tarehe 13 Novemba 1944, mtaa wa Uhuru, Tarafa ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam. Alisoma na kuhitimu Shule ya Msingi mkoani Dar es Salaam na baadaye kuendelea na masomo ya Sekondari katika Shule ya Sekondari St. Joseph Convert School, Dar es Salaam hadi alipohitimu Kidato cha Nne mwaka, 1963.

Marehemu Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu), alijiunga na JWTZ tarehe 07 Desemba 1964 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 22 Juni 1967. Alistaafu Utumishi Jeshini kwa Heshima tarehe 30 Juni 1999.

Katika utumishi wake Marehemu alishika Nyadhifa mbalimbali Ikiwemo Mkaguzi Mkuu wa Jeshi Makao Makuu mpaka anastaafu. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 20 Aprili 2017 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 10:30 Asubuhi.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents