Habari

Profesa Kitila awamwagia sifa Dawasco na kutoa agizo hili….

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amewamwagia sifa Kampuni ya Usambazaji wa Maji Dar es Salaam (DAWASCO) pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, huku akitaka mamlaka hiyo kuongeza kasi ya usambazaji na upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo

Profesa Kitila Mkumbo, wakati akiongea na Menejimenti ya Mamlaka hizo Jijini Dar es Salaam alisema, “Nawapongeza sana Dawasco kwani mnafanya kazi kubwa sana. Binafsi nimekua nikiwafuatilia hata kabla sijaingia katika wizara hii. Kwakweli mnafanya kazi kubwa na mnastahili kupongezwa. Muendelee hivyo hivyo kwani watu wanahitaji maji na si vinginevyo.”

Aliongeza kwa kusema, “Pamoja na kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha upatikanaji wa maji unakuwepo, hakikisheni mnaongeza kasi ya usambazaji wa huduma hii muhimu kwa wananchi wa Tanzania, mkifanya hivyo mtakuwa mnatendea haki dhana ya kuwa mnaongoza kwa mapato lakini pia mnatoa huduma stahiki kwa wananchi.”

Aprili 4 mwaka huu, Rais Magufuli alimteua Profesa Kitila Mkumbo, (ACT -Wazalendo), kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents