Habari

Temba, Juma Nature na Chege warudishwa pamoja na P Funk Majani, ni TMK ? (Video)

 

Wasanii waliofanya vizuri katika game ya muziki @chegechigunda , @mhtemba pamoja na @sir_nature wiki hii wameonekana wakiwa pamoja studio na producer @majani187 baada team hiyo kutengana kwa muda mrefu.

Wasanii hao walifanya kazi kwa pamoja katika kundi la TMK kwa mafanikio makubwa kabla ya kugombana na kila msanii kufanya kazi kivyake.

Taarifa zilidai wasanii hao waligombana na hawakuwa wanawasiliana kabisa.

Katika video hii wasanii hao wakiwa na producer Majini wameoneka kuwa na chemistry ya pamoja hali ambayo imeonyesha huwenda kukawa kunakitu kikubwa kinakuja.

Bongo5 inafanya jitihaza za kuzungumza na wasanii hao ili kujua nini kinaendelea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents