Tiba mbadala zitumike hospitali – Prof. Ndalichako

Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imeshauri tiba mbadala ziingizwe kwenye mfumo rasmi wa matibabu nchini katika kutibu magonjwa yasiyoambukiza.

Wadau mbalimbali wa Afya waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo.

Hayo yameelezwa katika hotuba ya Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako, iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe, katika ufunguzi wa Kongamano la tatu la Kuzuia na Kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.

Katika hotuba hiyo, Prof. Ndalichako amesema kwamba taasisi zinazoshughulika na utafiti zinatakiwa kufanyia uchunguzi wa dawa mbadala na ziboreshwe ili ziweze kutumiwa katika hospitali nchini.

Akizungumzia magonjwa yasiyoambukiza yanayotibiwa kwa njia mbadala kama Pumu, na Shinikizo la juu la damu na mengineyo, Prof. Mdoe amesema tafiti zaidi zifanyike na zitumiwe na wataalamu.

Mbali na hayo hotuba ya Prof. Ndalichako imesisitiza watafiti wanapaswa kuwaza kimataifa ili kutatua changamoto za nchi na diyo kutegemea tafiti za nje ambazo haziendani na mazingira halisi ya nchi.

Mbali na hayo Naibu Katibu Mkuu, Prof. Mdoe amesisitiza tafiti zinazofanywa na wataalamu zisiishie kwenye maandishi pekee, badala yake zinapaswa kuleta mabadiliko chanya.

Kuhusu Sekta ya Afya nchini, hotuba ya Waziri Ndalichako imeeleza kuwa chini ya Rais Samia Suluhu itafanya kazi na wadau wote wa Afya ili kuhakikisha namba za magonjwa na vifo vinapungua kutokana magonjwa yasiyoambukizwa.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button