Siasa

Timu ya Serengeti girls yaweka historia mpya Bungeni, wachezaji wakalia viti vya Wabunge (+ Video)

Timu ya Wasichana ya Tanzania chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imeweka historia ya kuwa timu ya kwanza kuingia na kukaa eneo maalumu wanalokaa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata mwaliko Bungeni baada ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia India 2022.

Kikosi cha Serengeti Girls wakiwa Bungeni leo,Dodoma

Nahodha Serengeti Girls Noela Patrick amesema mafanikio waliyoyapata ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia ni ushindi wa kwa  Watanzania wote na kila Mtanzania anapaswa kujivunia ushindi huo huku akimshukuru Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa kwa timu hiyo.

Ushindi huu umechochewa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa bega kwa bega na timu zote za Taifa na tunamuahidi Rais kwamba kama anavyoupiga mwingi na sisi tutakwenda kuupiga mwingi India”amesema Noela

Serengeti Girls imefuzu michuano ya kombe la dunia chini ya miaka 17 zitakazofanyika nchini India 2022 kuanza Oktoba 11 -30,2022 huku wakiungana na Nigeria na Morocco kuwakilisha bara la Afrika kwenye fainali hizo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents