FahamuHabari

Tukio la Mamba kuuliwa na raia wa kigeni, TAWA waanza uchunguzi

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
(TAWA) imesema inaendelea na uchunguzi kuona
kama kuna ukiukwaji wa Sheria za uwindaji baada ya kuonekana kwa video ya Mwindaji wa Marekani Josh Bowmer akifurahia kuwinda mamba mkubwa nchini
Tanzania mwenye rekodi ya dunia na kuleta taharuki.

Taarifa yao inaeleza kuwa:-

“Hivi karibuni katika mandao wa kijamii wa Twitter imesambazwa picha jongefu (Video clip)
inayoonyesha mtu akifurahia kuwinda mamba mkubwa chini Tanzania mwenye rekodi ya
dunia. Tarifa hiyo imeleta taharuki kwa Umma.
TAWA inapenda kuufahamisha Umma kuwa uwindaji wa kitalii hufanyika kwa kuzingatia
Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Sura ya 283 pamoja na Kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2015 na marekebisho yake ya mwaka 2017, 2019 na 2020. Uwindaji wa kitalii pia husimamiwa na Mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyohatarini kutoweka (Convention on International Trade In Endangered Species of Wild Fauna and Flora – CITES) ambao Nchi yetu imeridhia. Mamba ni miongoni mwa
wanyamapori wanaolindwa na Mkataba huu na wamewekwa katika kundi la pili (Appendix
Il) ambalo linaruhusu matumizi ya uvunaji ikiwemo uwindaji wa kitalii.
Masharti ya uwindaji wa mamba kwa mujibu wa Kanuni na Mkataba wa CITES ni
kuhakikisha:
(i) Mamba wote wanaowindwa chini hawazidi 1,600 kwa mwaka;
(ii) Mamba anayewindwa ana urefu usiopungua sentimita 300;
(iii) Vibandiko maalum (Skin tags) vinafungwa katika ngozi za mamba wanaowindwa;na (iv) Vibali vya CITES (CITES export permit) vinatumika kusafirisha nyara zitokanazo na
mamba waliowindwa.
Chini ya Sheria na Mkataba huo, mtu yeyote anaruhusiwa kufanya uwindaji wa kitalii baada
ya kupata kibali kutoka TAWA na kutimiza masharti kama ilivyobainishwa hapo juu.

Mara baada ya uchunguzi kukamilika tarifa kamili
itatolewa na hatua za kisheria zitachukuliwa iwapo ukiukwaji utabainika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents