Burudani

Tumepata feedback ‘Game’ inafanya vizuri sana kwenye nchi nyingi Afrika – Nahreel

Producer na msanii wa Navy Kenzo, Nahreel amekiri kuwa ngoma yao ‘Game’ ndio imefungua njia waliyohangaika kuitafuta kwa muda mrefu.

navy

Ndani ya mwezi mmoja toka waiachie, ‘Game’ imeweza kukamata chati mbalimbali za Radio na Tv sehemu nyingi Afrika. Imeshika namba moja kwenye chati za vituo hivyo ikiwa ni pamoja na Top Ten East ya Soundcity TV.

Akiongea na EATV Nahreel amesema kuwa tayari wamepata feedback kutoka Nigeria, Ghana, Afrika Kusini, Zimbabwe, Kenya, na Uganda kuwa ‘Game’ inafanya vizuri sana kwenye nchi hizo.

Ameongeza kuwa matokeo hayo yametokana na bidii na juhudi waliyoiweka kwa muda mrefu.

Sept 9, Navy Kenzo walipost picha Instagram wakifanyiwa mahojiano na Soundcity Tv ya Nigeria jijini Dar, ikiwa ni ishara ya kukubalika zaidi Nigeria.

navy soundcity

“Shukrani za dhati kwao @soundcityafrica kwa kufanya maojiano na Navy Kenzo kuhusiana na muziki na nyimbo ya #Game ft @vanessamdee kushika namba moja kwenye chat za #EastAfricaMusic..” – Navykenzoofficial

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents