Habari

Tunaushukuru uongozi wa hospitali ya Nairobi – Mbowe

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa ana ushukuru uongozi wa hospitali ya Nairobi kwa kutoa ulinzi wa ziada kwaajili ya Mhe. Lissu kwa masaa 24 ndani na nje.

Akizungumza leo Ijumaa jijini Dar es salaam, Mbowe amesema mbunge huyo yupo chini ya ulinzi mkali sana huku akiwatoa hofu wananchi kuwa madaktari wamewahakikishia kuwa mbunge huyo atapona na kurejea katika hali yake.

“Nipende kusema tunawashukuru sana uongozi wa hospitali ya Nairobi, wenzetu walielewa hofu yetu na wametoa ulinzi wa ziada kwa ajili ya Mhe. Lissu masaa 24 ndani na nje. Kwa hiyo Lissu yupo chini ya uangalizi mkali sana, na hili lilifanyika kwaajili ya hofu iliyotanda na inayotanda kwa halali kabisa kwa sababu kuna watu walitaka kuondoa maisha ya Lissu lakini hawakuweza kufanikisha kazi yao, na hao watu hawata sita kuutelekeleza kama tutawapa nafasi hiyo kazi yao”, amesisitiza Mbowe.

Kwa upande mwingine, Mbowe amewataka wanachama wa chama hicho pamoja na watanzania kwa ujumla kutokuwa na hofu kuhusu Tundu Lissu kwani madaktari wameshawahakikishia kuwa Lissu atapona na kurudi kuendelea na harakati zake.

Jana Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alisema serikali ipo tayari kumtibia Mhe. Lissu popote pale duniani atakapo taka kwenda endapo itapata maombi kutoka kwa familia na madaktari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents