Habari

Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya wakanusha taarifa ya wajumbe wa Kenyatta kuzuiliwa kutua Tanzania

Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya umekanusha taarifa kuwa Ujumbe rasmi uliomuwakilisha Rais Uhuru Kenyatta katika msiba wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ulizuiwa kutua nchini.

Ujumbe huo ulioongozwa na Samuel Losuron Poghisio ulilazimika kurejea jijini Nairobi kwasababu ya hitilafu ya ndege ambapo Mamlaka za Tanzania zilipewa taarifa.

Ubalozi umesema taarifa hizo za upotoshaji, za uongo na zenye lengo la kuzorotesha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya iliyotangaza siku 3 za maombolezo kufuatia kifo cha Mzee Mkapa.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kenyatta alimuelezea Rais Mkapa kama shupavu aliyetetea maslahi ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents