Burudani

Uchambuzi wa Nikki wa Pili Bongo Flava kukosa tuzo na albamu (+video)

Rapper kutoka kundi la Weusi, Nikki wa pili amefunguka umuhimu wa tuzo na albam katika muziki wa Bongo Flava mara baada ya vitu hivyo kukosekana kwa sasa.Nikki amesema Tuzo zilikuwa na mchango mkubwa kwa wasanii kwani katika kuwakuza na kutoa kipimo cha ukuaji kwa kila mmoja.

“Tuzo zilikuwa zinamchango wake, zilikuwa zinamuongeza msanii CV, zilikuwa pia zinamuwezesha msanii kujua nafasi yake katika game kama ni mpya amekuja akapata tuzo anapanda lakini pia kulikuwa na tour ile ilikuwa inaongeza kipato kwa wasanii” amesema Madee.

Pia Nikki amefunguka suluhisho la albamu baada ya wasanii kuacha kutoa kwa kuhofia mfumo mbovu wa uuzaji ambao mara nyingi umekuwa ukilalamikiwa kuwanyonja wasanii.

“Album niliongea na Max Malipo wanakuja na kitu kizuri wanakuja na mfumo wa kusambaza albamu kwa sababu Max nchi nzima wana mawakala 16,000 kwa hiyo nimekaa nao huo mfumo nimeshauona kwa hiyo nafikiri mkombozi ameshapatina ni kusubiri tu uzinduliwe” Nikki wa Pili ameiambia Bongo5,

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents