Burudani

Uchebe ‘fake’ amkera Shilole

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva,  Shilole amemua kumtolea uvivu  mtu anayetumia jina la mpenzi wake wanaozusha stori za kuachana.


Hatua hiyo imekujaa baada ya mtu mmoja katika mtandao wa Instagram kutengeneza akaunti yenye jina la mpenzi wa mrembo huyo’Kigori’ kwa kuandika vitu vinavyashiria  wapo katika mgogoro wa kimapenzi.

“Plzzz plzzzzz mchumba wangu hana acount yeyote instagram naombeni mnaotumia jina la mchumba wangu sipendi maana mnaandika vitu ambavyo havipo kaka wa watu hata mambo ya mitandao na wala hajui mambo ya insta plzzzz ww unaetumia jina la uchebe vibaya Mungu anakuona @official_uchebe acha uongo tafuta folowas kwa njia nyingine ok na acount ya mchumba wangu ni hii @uchebe1 hizo zingine hatuzijui mkomeee,” ameandika Shilole katika mtandao wa Instagram.

Kumekuwa na tabia ya watu kutengeneza akaunti ‘Fake’ za mstaa katika mitandao ya kijamii jambo linaloweza kuhatarisha usalama wa watu hao na kusababisha kuto aminika pindi wakitoa taarifa, jambo ambalo limelalamikiwa na mastaa wengi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents