Habari

Uchumi wa Marekani washuka kwa robo ya pili mfululizo

Uchumi wa Marekani umeshuka kwa robo ya pili mfululizo ya mwaka, ishara ambayo katika nchi nyingi duniani inazingatiwa kuwa mdororo wa uchumi.

Hata hivyo kushuka huko kwa kiwango cha asilimia 0.9 katika kipindi cha miezi mitatu hadi mwezi wa Julai kumesababisha wasiwasi juu ya uchumi wa nchi hiyo.

Bei za mahitaji ya kila siku ikiwa pamoja na za chakula na mafuta ya petroli zinapanda haraka kwa kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu mwaka 1981.

Licha ya benki kuu ya Marekani kupandisha viwango vya riba ili kuzuia kupanda gharama za maisha bado pana hofu huenda nchi hiyo imeshaingia katika mdodoro wa uchumi hali inayotokea katika nchi ikiwa uchumi haustawi kwa muda wa robo mbili za mwaka mfululizo. Hata hivyo rais Joe Biden amesema uchumi wa nchi yake unaendelea kuwa imara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents