Habari

Uingereza yaanza harakati zake za kibiashara barani Afrika waziri Mkuu atua Kenya

Uingereza yaanza harakati zake za kibiashara barani Afrika waziri Mkuu atua Kenya

Theresa May na mtihani wa Uingereza kuboresha biashara na Afrika baada ya kujitenga na Umoja wa Ulaya,nchin ya Uingereza ina uhusiano wa kihistoria na mataifa mengi ya Afrika. Uhusiano huo bado unaendelea kuwa na maana, lakini kitu kimoja ambacho Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekutana nacho katika ziara yake ya Afrika ni kuwa nchi yake inagombea nafasi na mataifa mengine yanayowekeza kwa kiwango kikubwa.

Hii leo Bi May ametua Kenya baada ya kuzuru Afrika Kusini na Nigeria. Hii ni ziara ya mwanzo kwa Bi May barani Afrika akiwa mamlakani. Nchi yake imenuwia kuimarisha mahusiano yake na mataifa ya Afrika kipindi hiki ambacho wanakaribia kujitenga na Umoja wa Ulaya (EU).

Akiwa jijini Cape Town, Bi May ameahidi nchi yake kuwekeza pauni bilioni 4 barani Afrika mara baada ya nchi yake kuondoka EU mwakani.

May pia amesema anatarajia kusain makubaliano na serikali ya Kenya kurejesha mabilioni ya pesa yaliyotoroshewa Uingereza kinyume cha sheria.

“Azma ya Uingereza baada ya kujitoa EU mwezi Machi 2019 ni kuimarisha ushirikiano wake na dunia kwa ujumla…Wiki hii natarajia kuwa na mjadala wa namna gani wa kufikia azma hiyo pamoja na bara la Afrika kwa kusaidia katika uwekezaji wenye tija na kukuza ajira pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama,” ilisema sehemu ya taarifa ya Bi May kabla ya ziara yake.
Hatahivyo, hilo linaweza kuwa jambo gumu.

Britain’s Prime Minister Theresa May smiles during a bilateral meeting with Colombia’s President Juan Manuel Santos at 10 Downing Street in London, November 2, 2016. REUTERS/Kirsty Wigglesworth/pool

Kabla ya May kuwasili Kenya, rais wa taifa hilo Uhuru Kenyatta alikuwa Marekani ambapo alifanya mazungumzo na rais Donald Trump na wawili hao kusaini makubaliano kadha ya kibiashara yenye thamani ya $900 miloni.

Baada ya kukutana na Bi May, Bw Kenyatta ataelekea Uchina kwenda kushiriki mkutano wa uhusiano baina ya Uchina na Afrika.
Uingereza kwa sasa inabadili sharia zake ili kuruhusu bidhaa kutoka Afrika zinaingia nchini humo kwa namna sawa kama ilivyo sasa hata baada ya kujitenga na EU
Nchi za Afrika, nyingi zikiwa makoloni ya zamani ya Uingereza zitalazimika kujipanga upya katika uhusiano wao na nchi hiyo hususan baada ya kujitenga na EU. Endapo Uingereza itashindwa kuafikiana vizuri na EU kabla ya pande hizo mbili kutengana basi ni Dhahiri uhusiano wa kibiashara baina ya Uingereza na Afrika pia utayumba.

“Kenya mathalan mzunguko wake wa biashara baina ya EU na Uingereza ni asilimia 50 kwa 50, hivyo basi inawabidi waingie makubaliano mazuri na pande zote mbili sababu inahitaji masoko yote hayo kuuza chai, bidhaa ghafi na mazao mengine,” mchumi Tony Waitima ameiambia BBC.
Kenya ndio nchi kinara kwa kuuza maua waridi (roses) katika Umoja wa Ulaya, na ni nchi ya tatu kwa kuuza maua kwa ujumla duniani. Kilimo cha maua kinategemewa moja kwa moja na watu 500,000 kwamujibu WA Baraza la Maua la Kenya hivyo kupata makubaliano mazuri kutoka pande zote mbili ni jambo muhimu zaidi.

Pamoja na juhudi za Uingereza kuishika Afrika kibiashara lakini ni wazi kuwa bara hilo kwa sasa linabembelezwa kutoka kila kona.

Chanzo BBC.

By Ally Juma

Related Articles

5 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents