Burudani

Ujumbe wa Q Chief kwa Chidi Benz: Hutakiwi kufa, chukua nafasi ya Ngwair

Msanii mkongwe wa muziki, Q Chief amemsihi rapa Chidi Benz kutorudia tena kutumia dawa za kulevya huku akidai yeye anamuona rapa huyo kama mrithi wa rapa Ngwair aliyefariki miaka kadhaa iliyopita nchini Afrika Kusini.

Muimbaji huyo ambaye alimsindikiza rapa huyo XXL ya Clouds Fm kutambulisha wimbo wake mpya ‘Muda’, amedai Chidi Benz ni rapa ambaye hatakiwi kufa kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.

“Huu mimi ni mwaka wa tano sijapata nafasi ya XXL kutambulisha wimbo wangu mpya,usiwaangushe ukitapa nafasi hasa hasa kwa wakati huu itumie vizuri,” alisema Q Chief. “Mimi nimejitolea kwa sababu nimempoteza Ngwair halafu nikaumizwa sana wewe unajua Ngwair alikuwa nani kwangu,”

Aliongeza,”Wewe unachukua nafasi ya Ngwair hautakiwi kufa, wewe ni bora kuliko marapa wengi sana, hii nafasi ni bahati kwako ukiitumia umetoboa,”

Chidi Benz amemshirikisha Q Chief katika wimbo wake huyo mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents