Habari

Upinzani washinda uchaguzi wa Rais, Shelisheli

Kiongozi wa Upinzani katika taifa dogo la visiwa vya Shelisheli Wavel Ramkalawan ameshinda uchaguzi wa Rais baada ya tume ya uchaguzi kutangaza matokeo rasmi hapo jana siku ya Jumapili.

Seychelles Elects Wavel Ramkalawan as New President - Bloomberg

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa maiak 59 ambaye pia ni kasisi wa kanisa la Anglikana amepata asilimia 54.9 ya kura na kufanikiwa kumwaondoa madarakani rais wa sasa Danny Faure.

Tume ya uchaguzi imesema Faure amepata asilimia 43.5 ya kura na chama chake cha USP ambacho kimeongoza visiwa vya Shelisheli tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1977 kimeambulia viti 6 pekee vya bunge.

Chama cha Ramkalawan kimeshinda viti 25 katika bunge lenye viti 34, ushindi unaokiwezesha kuwa na udhibiti kamili wa Bunge.

Katika hotuba fupi baada ya kutangazwa matokeo, Ramkalawan ametaja rais anayeondoka kuwa ni rafiki yake na kuahidi kuwa atamteua kama mshauri wake kusaidia kulijenga taifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents