Michezo

Mbappe kuipatia zawadi PSG kabla ya kuihama

Mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe, 21, amekusudia kuipatia klabu yake ya Paris Saint-Germain Football Club ubingwa wa Champions League kabla ya kuhamia kwenye timu nyingine kubwa maneno hayo ni kulingana na kiungo wa kati aliyeichezea PSG na ambaye sasa ni balozi wa klabu hiyo Youri Djorkaeff. (Goal)

Mbappe denies making PSG demands - AS.com

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala 26 ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Tottenham pamoja na Man United yuko katika mazungumzo ya kuandikisha mkataba mpya na klabu hiyo ya Itali. (Sky Sports)

Paulo Dybala

Mshambuliaji wa Poland Arkadiusz Milik, ambaye alikuwa tayari kujiunga na Juventus msimu ujao ataondoka Napoli mwezi Januari huku klabu za Tottenham na Everton zikimnyemelea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.. (Calciomercato via Mail)Kylian Mbappe

Klabu ya Sheffield United wanataka kumchukua beki wa Man United na Argentina Marcos Rojo 30, kwa mkopo mwezi Januari.. (Sun)

Manchester United ilikosa kumsajili beki wa RB Leipzig na Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 Dayot Upamecano – ambaye kwa sasa ana thamani ya £55m – kwasababu ya mgogoro kuhusu £200,000 miaka mitano iliopita . (Sun)

Arsenal ina hamu ya kumsajili kungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar, 22, lakini inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Paris St-Germain na Juventus. (Tuttosport – in Italian)Houssem Aouar

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anasema kwamba amekuwa wazi na kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, licha ya wakala wa mchezaji huyo kudai kwamba kumekuwa hakuna uwazi kuhusu mchezaji huyo kuwachwa nje ya kikosi cha timu hiyo.. (Mirror)

Liverpool Huenda ikaamua kutomsaini beki wa kati mwezi Januari na kusubiri mchezaji atakayedumu msimu ujao, licha ya jeraha baya lililompata beki wa Uholanzi Virgil van Dijk. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Luka Modric, 35, amesisitiza kwamba yeye ni mzee sana kufuata nyayo za mshambuliaji wa Wales Gareth Bale na kurudi Tottenham.. (FourFourTwo via Marca)Luca Modric

Winga wa Manchester City na Algeria Riyad Mahrez, 29, amekana madai katika vyombo vya habari vya Ufaransa kwamba alizungumzia uwezekano wa kujiunga na PSG. (Manchester Evening News)

Kiungo wa kati wa Newcastle na England Jonjo Shelvey, 28, anakabiliwa na jeraha la nyonga ambalo huenda akafanhyiwa upasuaji. (Newcastle Chronicle)

Kiungo wa kati wa Brighton na England Adam Lallana, 32, anasema kwamba alipogundua kwamba hahitajiki katika klabu ya Liverpool alitumia kila siku katika klabu hiyo kama ambaye ilikuwa siku yake ya mwisho. (Liverpool Echo)Adam Lallana

Juventus na Barcelona wana hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Ajax na Uholanzi mwenye umri wa miaka 19 Ryan Gravenberch, 18. (Tuttosport – in Italian)

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti ametaja matusi ya mitandao ya kijamii yaliowalenga wachezaji wake kama yasio ya haki na hayatakubalika .. (Liverpool Echo)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents