Burudani

Upo Hapo ya AY na Mwana FA yatua kwenye platform hii mpya ya Mkito

Ngoma kali ya wakali na legends wa Bongo Fleva nchini Tanzania ambao pia wanatamba nje ya Tanzania, Hamis Mwinjuma, Ambwene Yessaya na Fareed Kubanda inayokwenda kwa jina la “UPO HAPO” inapatikana exclusively kupitia Mkito App ambayo imezinduliwa rasmi weekend hii na inapatikana kwenye Playstore

Mwana FA, AY pamoja na Fid Q wakiwa katika uzinduzi huo.

Katika uzinduzi huo, Mwana FA alisema kwa sasa wameungana na kampuni ya Mkito kuanzisha label ambayo itakuwa inafanya kazi kawa level za kimataifa.

Mkito App inakuwezesha kusikiliza na kupakua nyimbo za wasanii wa ndani ya Tanzania na wa Kimataifa BILA KIKOMO katika ladha tofauti kama Afrobeat, Genge, Bongo Flava, Swahili Rap, Fusion, Jazz, Singeli, Taarab, Zouk, Soul, Reggae, muziki wa jadi, Beats, Mashairi na maudhui mengine ya sauti – popote ulipo.

Katika jambo ambalo Mkito wamefanya poa sana ni kuiwezesha App hiyo kucheza nyimbo ambazo umezitunza kwenye simu yako au au kadi ya kumbukumbu na kuhakikisha kuwa mzuka unaendelea popote unapoenda! Ipakue leo ufurahie kile ambacho umekuwa ukikosa.

Jinsi ya kupata Punguzo kupitia Coupon

  1. Pakua Mkito App kwenye simu yako
  2. Jisajili kwa kupitia barua pepe au akaunti ya mtandao wa kijamii
  3. Ongeza salio kwenye akaunti yako ya Mkito (MPesa/Tigo Pesa/Paypal)
  4. Jiunge na kifurushi (Ingiza code “UPOHAPO” unapojiunga upate punguzo la 50%)
  5. Furahia muziki bila kikomo popote ulipo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents