Michezo

Usain Bolt kupokonywa medali yake moja ya dhahabu ya Olimpiki

Usain Bolt atatakiwa kuirudisha moja ya medali zake tisa za Olimpiki baada ya mkimbiaji mwenzake wa Jamaica, Nesta Carter kugundulika alitumia madawa yalivyopiga marufuku.

Carter alikuwa sehemu ya timu ya Jamaica kwenye mbio za 4x100m kwenye mashindano ya Olimpiki ya Beijing, 2008. Alikuwa mmoja wa wanariadha 454 ambao sampuli zao zilipimwa upya na kamati ya kimataifa ya Olimpiki mwaka jana na kubainika kulikuwa na dawa ya kuongeza nguvu iliyopigwa marufuku ya methylhexaneamine.

Carter, 31, pia alikuwa mmoja wa wakimbiaji walioshinda miaka mitano iliyopita kwenye mashindano ya London na ameisaidia Jamaica kushinda mashindano ya kimataifa mwaka 2011, 2013 na 2015.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents