Michezo

Australian Open: Venus Williams atinga fainali

Venus Williams amemshinda Coco Vandeweghe na kufikia fainali za Grand Slam ya kwanza katika kipindi cha miaka minane kwenye michuano ya Australian Open.

Mchezaji huyo mwenye miaka 36, alikomaa na kumzidi nguvu Mmarekani mwenzake kwa 6-7 (3-7) 6-2 6-3 huko Melbourne, na hivyo kuwa na uwezekano wa kuja kukutana na dada yake Serena kwenye fainali.

Venus Williams, ambaye ni mchezaji nambari 13 duniani, alishindwa na dada yake kwenye fainali za Australian Open miaka 14 iliyopita.

Serena Williams, mchezaji nambari 2 duniani, atacheza na Croat Mirjana Lucic-Baroni kwenye nusu fainali ya pili.

Akipata ushindi, hiyo itakuwa ni fainali ya tisa ya mabinti wa Williams kwenye Grand Slam – ya mwisho ikiwa ni ile ya Wimbledon mwaka 2009.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents