Habari

Utafiti: Pato la Taifa kukuwa kutokana huduma za fedha za simu za mkononi

Utafiti mpya kutoka kwa kampuni ya Vodafone Group, Vodacom Group, Safaricom na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP, United Nations Development Programme) unaonyesha kuwa uenezaji na matumizi fanisi ya huduma za fedha za simu za mkononi yanahusishwa na athari nzuri ya moja kwa moja kwa ukuaji wa Kiwango cha Uchumi (GDP) katika masoko yanayokua kwa sababu husaidia biashara kupunguza gharama, kupata mkopo wa kuwekeza na kuwasiliana na wateja ambao hawakuwa na uwezo wa kufikia huduma za fedha hapo awali.

Sitoyo Lopokoiyit, Afisa Mkuu Mtendaji wa M-Pesa Africa na Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha katika kampuni ya Safaricom

Utafiti wa mfano wa takwimu za uchumi1 – ambao ulichunguza nchi 49 barani Afrika, Asia na Amerika Kusini – ulibainisha kuwa nchi zilizokuwa na huduma fanisi za fedha za simu za mkononi zilikuwa na ukuaji wa Kiwango cha Uchumi kwa kila mtu kwa mwaka cha hadi asilimia 1 zaidi kuliko nchi ambako mifumo ya huduma za fedha za simu za mkononi hazikuwa fanisi au zilikuwa hazijaanzishwa.

Kulingana na utafiti wa awali wa Benki ya Dunia (World Bank) kuhusu uhusiano kati ya ukuaji wa uchumi na kupungua kwa idadi ya watu wanaoishi katika umaskini2, ukuaji huu wa Kiwango cha Uchumi (GDP) kwa kila mtu unamaanisha kuwa nchi zenye huduma fanisi za fedha za simu za mkononi zinaweza kupunguza umaskini kwa karibu asilimia 2.6.

Uchanganuzi huu ulifanywa kama sehemu ya kampeni ya makampuni ya Africa.Connected, mradi wa kuendeleza ukuaji endelevu kupitia ushirikiano na kusaidia kuondoa tofauti zinazozuia maendeleo katika sekta kuu za uchumi barani Africa. Matokeo haya ni sehemu ya utafiti mpya, Mifumo Dijitali ya Fedha ya Kuwezesha Watu Wote (Digital Finance Platforms to Empower All), utafiti wa nne uliotayarisha na kuchapishwa chini ya mwavuli wa utafiti wa Africa.Connected.
Sitoyo Lopokoiyit, Afisa Mkuu Mtendaji wa M-Pesa Africa na Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha katika kampuni ya Safaricom, alisema:

“Mifumo ya huduma za fedha za simu za mkononi kama vile M-Pesa ni viendeshaji muhimu vya usawa wa kufikia huduma za fedha katika jamii, hali ambayo inaweza kuboresha fursa za maisha ya mtu binafsi na kuwezesha biashara kuanzishwa na kupanuka, na kuleta utajiri na ajira katika uchumi unaokua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents