Habari

UTAFITI: Wanasayansi wagundua misuli ya mbwa anayotumia kupitia macho kumvutia binadamu 

Ukimuona mbwa anakuangalia ni kama anakwambia kitu au kutaka kujileta karibu nawe, huenda anatumia misuli maalum ya macho kuvuta hisia zako.

Watafiti wamebaini kuwa mbwa wana misuli inayowawezesha kugeuza macho yao ili kuwavutia wanadamu.

Musili hiyo maalum pia inawawezesha mbwa kubadilisha macho yao yakafanana na ya ”mtoto mchanga” ambayo inamfanya binadamu kumjali na kumpenda.

Kwa mujibu wa shirika la habari BBC,  Utafiti huo umegundua kuwa “macho ya madogo” inawafanya mbwa wanaofugwa kujenga uhusiano wa karibu na binadamu.

Tafiti zilizopita zinaonesha kuwa hali hiyo inawavutia wanadamu, lakini utafiti huu wa sasa kutoka Uingereza na Marekani unaonesha kuwa kumekuwa na mabadiliko ya kimaumbile katika macho ya mbwa ambayo inawawezesha kufanya hivyo.

Kope zinazoashiria ujumbe fulani

Mbwa anaweza kutumia kope zake kufanya kitu ambacho watafiti wanakiita “kope zinazotoa ujumbe ” na “kujenga hisia kuwa anaweza kuwasiliana kama mwanadamu”.

“Mbwa anapogeuza kope zake mara kwa mara anaashiria kuwa anata mwanadamu awe karibu nae,” anasema mmoja wa watafiti Dr Juliane Kaminski kutoka Chuo Kikuu Cha Portsmouth.Dog eyes

Misuli hiyo huwawezesha mbwa kufanya macho yao kuonekana’makubwa “, au kuyafanya kuonekana kama ya mtoto mchanga hali wanayofanya wakiwa na huzuni.”.

Anasema kuwa wanadamu huenda wakawa na hisia ya kuwajali mbwa hata bila ya wao kutumia misuli hiyo maalum hali ambayo inaweza kuimarisha zaidi uhusiano wa mnyama huyo na binadamu”

“Kuna ishara wazi kuwa mbwa walitumia misuli h iyo kugeuza kope zao baada ya kufugwa kama mnyama wa nyumbani aliyetokana na mbwa mwitu,”anasema Dr Kaminski, katika utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la kitaifa la sayansi nchini Mararekani.

Matokeo ya Utafiti huo kutoka Uingereza na Marekani yanaashiria kuwa maumbile ya uso wa mbwa yamebadilika kwa zaidi ya maelfu ya miaka tangua alivyoanza kuishi na binadamu.

Tafiti zilizopita zinasema kuwa mbwa watumia zaidi misuli hiyo kubadilisha macho yao na kuyafanya madogo wakati binadamu wanapowaangalia- kuashiria kuwa ni tabia wanayofanya makusudi kwa lengo la kuwavutia wanadamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents