Burudani

Video: Alikiba ajibu kuhusu kukopi ‘Seduce Me’

Msanii wa muziki Bongo, Alikiba ametoa majibu juu ya tetesi zinazosambaa kuwa wimbo wa ‘Seduce Me’ ameukopi.

Akiongea na Bongo5, Ali amesema kuwa ngoma hiyo ameifanya tangu miaka miwili iliyopita hivyo wanaosema amekopi waende wakaangalie hizo zinazodaiwa ameukopi.

“Seduce me ni muziki ambao umenifurahisha hata mimi mwenyewe, ni muziki ambao umenileta mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki kwa muda mfupi kwa sababu muitikio wake umekuwa mkubwa zaidi ni nyimbo nzuri sana watu wameipokea. Ukiingalia imezungumziwa na watu wengi kila aina ya viongozi, mabloger na waandishi wa habari,” amesema Kiba.

Ali ameongeza, “Unajua muziki mzuri mara nyingi unazungumziwa na lazima kushambuliwe na vitu kama hivyo. Kuna watu wachache ambao hawaniamini kama naweza kufanya muzuki kama huo ni kwa sababu ya mabadiliko na jinsi gani nafanya muziki yangu tofauti. ‘Seduce Me’ ni kati ya muziki ambao ni tofauti kabisa mimi kuintroduce Tanzania kati ya miziki yangu yote na nimerekodi karibu miaka miwili toka studio ya zamani ya Man Walter na vile vile haitowahi kutokea na siwezi kufanya vitu kama hivyo kwa sababu najiamini sana talent yangu. Kitu ambacho nafanya always ni kufanya kitu kizuri harafu ma fans wanakuja kupokea,” amesema Alikiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents