Burudani

Video: Kutana na Kundi ‘Sauti From East’, wakali wapya wa Pop TZ

Kundi jipya la muziki wa Pop, Sauti From East linaloundwa na vijana wawili, Chris Daniel na Chris Ringson, ilimetangaza ujio wake mpya katika tasnia ya muziki nchini.

Waimbaji hao ambao wanafanya vizuri na wimbo wao mpya ‘Someone Else’, wamedai ujio wao ni kutaka kutoa burudani ya muziki wa Pop.

Wakizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, wasanii hao wamedai wameamua kufanya muziki wa Pop kwa kuwa wana uwezo wa kuimba na pia ni muziki ambao unapendwa na watu wengi duniani.

“Sisi kabla ya kuamua kuwa kundi tulijifikiria tuje kwa mtindo gani, kila mmoja anajua uwezo wa mwenzake, kwa hiyo hakikuwa kitu kigumu kuamua tufanye nini kwa sababu ni watu ambayo tumejuana toka tukiwa wadogo mpaka tunamaliza chuo tupo pamoja. Pia kwenye suala la muziki kama nilivyosema, sisi wote tunajuana, sauti zetu tunazijua, tukaona ni jambo jema kama tukiamua kufanya muziki wa Pop kwa sababu ni muziki ambao tunaweza kuufanya vizuri kwa kiwango cha kimataifa,” alisema.

Kundi hilo linajipanga kuachia video ya wimbo wao mpya uitwao, ‘Someone Else’.

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents