Burudani

Lil Wayne akatisha show ghafla jukwaani, baada ya sauti iliyosikika ‘piga risasi’ kusambaa ukumbini

Rapper Lil Wayne kutoka Marekani usiku wa kuamkia leo amejikuta akikatisha Show yake ghafla mjini Atlanta baada ya sauti iliyosikika ikiita ‘Piga Risasi’ kusambaa kwenye ukumbi ambao alikuwa anafanya show.

 

Sauti hiyo ambayo haikutambulika, ilipeleka watu waliohudhuria show hiyo ya tamasha la A3C kushikwa na taharuki na kuanza kukanyagana wakigombania kutoka nje.

Zaidi ya watu mia moja wamepata majeraha kwenye tukio kutokana na kukanyagana huku watatu wakianguka kwa mshtuko.

Hii ni show ya kwanza kwa Lil Wayne kufanya tangu aachie Album yake ya ‘Tha Carter V’ wiki iliyopita.

SOMA ZAIDI-Lil Wayne aiachia album yake ya ‘Tha Carter V’, baada ya vuta nikuvute na Cash Money

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents